Joshua 1:13-15

13 a“Kumbukeni agizo lile Musa mtumishi wa Bwana alilowapa: ‘Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa ninyi raha, naye amewapa nchi hii.’ 14 bWake zenu, watoto wenu na mifugo yenu watakaa katika nchi ile Musa aliyowapa mashariki ya Yordani, lakini mashujaa wenu wote, wakiwa wamevikwa silaha kikamilifu lazima wavuke mbele ya ndugu zenu. Imewapasa kuwasaidia ndugu zenu hadi 15 c Bwana awape nao raha, kama alivyokwisha kufanya kwa ajili yenu hadi wao pia watakapokuwa wamemiliki nchi ile Bwana Mwenyezi Mungu wenu anayowapa. Baada ya hilo, mwaweza kurudi na kukalia nchi yenu wenyewe, ambayo Musa mtumishi wa Bwana aliwapa mashariki mwa Yordani kuelekea linakochomoza jua.”

Copyright information for SwhKC